Televisheni

TV ya Kijerumani ya mwaka wa 1956.
TV ya Kijerumani ya mwaka wa 1956.

Televisheni (pia: TV, telly au tyubu) ni chombo (kifaa) chenye kiwambo au kioo ambacho kinapokea mawasiliano kutoka katika kituo cha televisheni na kuyabadilisha kuwa picha na sauti. Neno "televisheni" linatokana na neno tele (kutoka Kigiriki: kwa mbali sana) na Kilatini vision (kuona), kwa pamoja inaunda neno tele-visheni.

[hariri] Historia ya televisheni

TV Braun HF 1 ya Kijerumani ya mwaka wa 1959.
TV Braun HF 1 ya Kijerumani ya mwaka wa 1959.

Kikawaida TV inaonekana kama sanduku. TV za zamani kabisa zilikuwa zina kirimba au fremu kubwa ya mbao na zilikuwa zikiwekwa chini kama fanicha. TV za kisasa ziko za namna nyingi kama zilivyo nyingi zaidi. Kuna baadhi ya TV zinaweza kunea mkononi mwako na zikawa zinaendeshwa kwa kutumia mabeteri.

TV zingine zinaweza kuena ukuta mzima wa nyumba, na inaweza kukaa katika sakafu, au kuna zingine ambazo zimenyooka (flat) na zinaweza kubandikwa ukutani. Televisheni inaweza kuonyesha picha kutoka sehemu mbalimbali. Cha kwanza unachotakiwa kufanya ni kutumia kidaka mawasiliano au antenna (au aerial), hii itaonyesha maonyesho yote yanayorushwa na kituo cha matangazo ya televisheni.

Vituo vya TV vinaweza kuwa mbali kabisa lakini bado matangazo yake yanapatikana kama antena ya kurusha mawimbi yake iko katika umbali wa kilomita 50 hadi 150. Teknolojia mpya zaidi ni kutumia vyombo vya angani kama antena ya kurusha mawimbi haya duniani. TV pia inaweza kuonyesha filamu kutoka katika VCD na DVD au VCR yaani tepu za kawaida. Cable TV na Satellite TV zinaweza zikatoa huduma nyingi ya vipindi vya TV kwa mara moja na vilevile kuvirusha hewani. Video game nyingi huunganishwa katika TV ili uweze kuona kile unacho kicheza. Kuna baadhi ya tarakilishi au kompyuta ambazo unaweza kutumia TV kama kioo cha kufanyia kazi zako au kwa jina lingine monitor.

TV zote zina kioo ambacho kinaonyesha picha. Kabla ya miaka ya 1970 TV zilikuwa hazina rangi ( yaani "#FFFFFF and #000000"), ambazo zilikuwa zinafanya kila kitu kionekane cha rangi ya kijivu. Lakini kwa sasa karibuni TV zote zinaonyesha na rangi. Kawaida ya viwambo vingi (kioo au vioo) vingi huonyesha kuwa vina kona ya mzunguko, lakini kwasasa vioo vingi hutengenzwa kwa kunyooka na zina ncha pembeni.

Njia ya picha katika TV
Njia ya picha katika TV

Kabla ya miaka ya 1990, TV zote zilikuwa zikitengenezwa kwa umbo moja-zilikuwa kubwa kidogo na kisha zilikuwa ndefu. Kwa mfano, kama kioo kilikuwa cha urefu wa ichi 3, basi lazima itakuwa na upana wa inchi 4. Au kama kioo kina urefu wa cm 30, lazima kitakuwa kina upana wa cm 40.

Umbola TV za kisasa zinazidi kuwa maarufu na kupata wapenzi wengi zaidi kila siku ziendapo. TV zenye kioo cha upana mkubwa wa mstatili huonekana vizuri katika luninga kubwa (theatre screen) na pia inapenzi wengi kuliko. Hizi huzita kioo kipana (au kwa kiing: widescreen). Endapo TV ya kioo kipana kina urefu wa cm 30, basi lazima itakuwa inaupna wa cm 53. Ili ifanye kazi vizuri, uonyeshaji wa TV pia unatwakiwa ujengwe kwa namna ya upana yaani widescreen. Kioo kipana kinaweza kubadilishika kwa ukubwa wowote unaoutaka, lakini swala la umbo linabaki kuwa vilevile kama lilivyo (Widescreen).

[hariri] Viungo vya nje

Jua habari zaidi kuhusu Television kwa kutafuta kupitia mradi wa Wikipedia Sister
Uchambuzi wa kamusi kutoka Wikamusi
Vitabu kutoka Wikitabu
Quotations kutoka Wikidondoa
Source texts kutoka Wikichanzo
Images and media kutoka Commons
News stories kutoka Wikihabari
Learning resources kutoka Wikichuo

Budowa skrzyni biegów,książka wynajem samochodów pyrzowice opisy gg mieszkania Szczecin odżywki ustka Zespoły muzyczne nauka jazdy kraków mieszkania wrocław Katalog Branżowy Firm Usługi Yerba mate Lokówki, prostownice Efect Doradztwo Finansowe Nieoficjalne Centrum Siemens zakłady bukmacherskie kick koparki Bułgaria wczasy Karaoke expekt COOLsurf