|
VifaaLugha nyingine
|
Martin LutherMartin Luther (10 Novemba, 1483 – 18 Februari, 1546) alikuwa Mkristo mwanateolojia kutoka nchi ya Ujerumani. Alijiunga na shirika la watawa wa mtakatifu Augustino, akawekwa wakfu kama padri na kuwa profesa wa Biblia kwenye chuo kikuu cha Wittenberg. Swali lililomtesa kwa muda mrefu, yaani "Vipi nimpate Mungu mwenye huruma?", lilijibiwa aliposoma Waraka kwa Waroma, sura ya 3, mstari wa 24: "kwa zawadi ya neema ya Mungu, watu wote hukubaliwa kuwa waadilifu kwa njia ya Yesu Kristo anayewakomboa." Hapo alianza kupinga bidii zote za kanisa za kuwakomboa watu kupitia matendo au sadaka zao (rehema). Tarehe 31 Oktoba, 1517, alitolea "Hoja 95 dhidi ya madekezo" (kwa Kijerumani: 95 Thesen wider den Ablass) kimaandishi. Hii ilimfanya ashindane hata na Papa wa Roma, na kutengwa na Kanisa Katoliki akiongoza Matengenezo ya kiprotestanti yaliyosababisha mapema madhehebu mengi mapya kutokana na wazo kuu la kwamba Biblia inajitegemea na kumtosha kila anayesoma. Aliandika vitabu vingi, kutunga nyimbo kadhaa na hasa kutoa tafsiri Biblia katika lugha ya Kijerumani. Athari yake imekuwa kubwa sana katika Kanisa na ulimwengu kwa jumla.
|