|
VifaaLugha nyingine
|
Japani
Japan ni nchi ya visiwa katika Pasifiki mbele ya mwambao wa mashariki ya Asia. Wajapani wenyewe hutumia jina la "Nihon" au "Nippon" lenye maana ya "Mwanzo wa jua". Hivyo Japani huitwa pia "Nchi ya Macheo". Nchi ina eneo la 377.000 km² na wakazi milioni 128. Japani ni kati ya nchi za dunia zilizoendelea sana kiuchumi, kiteknolojia na kisayansi. Ilikuwa nchi ya kwanza nje ya Ulaya iliyofaulu kujenga jamii ya viwanda.
[hariri] JiografiaJapani ni funguvisiwa yenye visiwa zaidi ya 3.000 mbele ya pwani la Uchina, Korea na Urusi (Siberia). Visiwa vikubwa na muhimu zaidi ni vinne tu ndivyo Honshu, Hokkaido, Shikoku na Kyushu. Safu ya milima inapita visiwa vyote vikubwa na kusababisha msongamano makubwa ya wakazi katika miji kutokana na uhaba wa ardhi ya kukalia. Hali halisi Japani yote ni safu ya milima tu inayopanda juu kutoka msingi wa bahari na vilele vya milima yake huonekana juu ya uso wa bahari kama visiwa vikubwa au vidogo. Kijiolojia eneo hili liko kwenye mstari ambako mabamba ya gandunia ya Ulaya-Asia, Pasifiki na Ufilipino hukutana. Hii ni sababu ya kuwepo kwa volkeno 240 katika Japani na takriban 40 kati ya hizo ni hai pia kutokea kwa matetemeko ya ardhi ya mara kwa mara. Hivyo Japani ni sehemu ya pete la moto la Pasifiki linalozunguka bamba la Pasifiki. Japani inapatwa kila mwaka na dhoruba kali aina ya taifuni. Hata tsunami (ni neno la Kijapani) ni kawaida. Nchi inajikinga na mitambo mengi ya kutoa taarifa ya tsunami kuanza pia mitambo ya kufunga milango ya mabandari. [hariri] MijiWajapani wengi hukalia sehemu ndogo ya 10% za nchi. Kuna miji kumi yenye wakazi zaidi ya milioni moja. Miji mikubwa ni Tokyo, Yokohama, Nagoya, Osaka, Kyoto, Kobe, Hiroshima, Fukuoka, Kitakyushu, Sendai na Sapporo. Usafiri ndani ya Japani ni hasa kwa treni, mabasi na ndege. Treni ya Shinkansen visiwani Honshu na Kyushu ni kati ya treni zenye mkasi mkubwa duniani. [hariri] Mikoa
[hariri] Historia[hariri] Uchumi[hariri] Utamaduni[hariri] Dini
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||